Tuesday, October 29, 2013

Rozi ni binti anaeishi na bibi yake mtaa wa mwangata mkoani Iringa leo hii amekutana na mlatibu wa kikundi cha Miale sanaa Group Timoti John katika mtaa wa gangilonga nakuanza kumwelezea shida yake kuwa anaitaji kujiunga na kikundi cha Miale sanaa Group nakudai kwamba kilicho mfanya ajiunge nikutokana na kushawishika na filamu iliyo tolewa na kikundi hicho inayokwenda kwajina la Zero Done nakusema kwamba yeye anakipaji ila ilikuwa hajuwi aanzie wapi ila aliposikia mahojiano katika rodio ambapo Khamis Nurdin mkurugenzi wa kikundi cha Miale sanaa Group alipotoa ruksa ya watu kujiunga nayeye ndio akakitafuta kikundi kilipo nakujalibu kukutana na viongozi anasema haamini kama leo kakutana na viongozi hao nakisha akaelezea historia yake kwa kifupi kuwa yeye nimtoto wa mwisho katika famila ya watoto nane ila watano wamefaliki katika njia ya kutatanisha Rozi katika kipengele hichi aliongea kwauzuni sana alisema kwamba ndugu zake walianza kupukutika baada ya baba yao kupotezwa na mjomba yao kisha na wao wakaanza kupotea mmojammoja ingawa walikuwa wamechangia mama ila ilimuuma sana imani ya kishilikina ndio iliyo wapoteza ndugu zake nakudai kwamba yeye hadi sasa ham,juwi baba yake mzazi huwa anasimuliwa kuwa baba yake alipotea katika njia za utata Timoti John alimuuliza juu ya elimu yake Rozi akadai ameishia la saba naalishindwa kuendelea na masomo kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu yeye na bibi yake kwani mama yake alifariki pia, ndipo Timoti John alipo amuwa kumtafuta Khamis Nurdin kumweleza juu ya kumsaidia Rozi nakumfata kwapamoja alipo

Timoti John akimsikiliza kwa umakini sana Rozi nakumwambia asijari atasaidiwa ngoja wa mfate Khamis Nurdin ili wamweleze hili

Khamis Nurdin akiwa anawasubiri Timoti John na Rozi katika gari la dada yake aitwae mwasiti

Khamis Nurdin akiwa anamsikiliza Rozi kwa umakini  baada ya kufika Rozi alimweleza Khamis pia juu ya shida yake nakusema anaomba asaidiwe juu ya sanaa na pia anafani ya ufundi cheleani anaomba apate mtu wa kumsaidia mashine ya cheleani ili ajiajili kupitia mashine hiyo Khamis Nurdin ambae ni Mkurugenzi wa kikundi cha Miale sanaa Group alimkubalia kujiunga na kikundi hicho na kumwahidi kumsaidia katika sanaa 

Rozi akimshukuru Timoti John kwa kukubaliwa kujiunga na kikundi hicho

Khamis Nurdin akijipiga picha yeye na Rozi baada ya kumaliza maongezi

0 comments:

Post a Comment